Bofya Kitufe Hapa Kutufollow Facebook na twitter Radio Kwizera.

Radio Kwizera

Jukwaa la Matumaini - Sowing Seeds of Hope

Ngara 97.9 FM Bukoba 97.7 FM Kasulu 94.2 FM Kahama 97.3 FM Geita 90.5 FM Kibondo 93.6 FM
 • JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  OFISI YA RAIS

  TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

   

  Anwani ya Simu: “REGCOM”

  Simu ya mdomo: (028) 2220215-18

  E-mail: [email protected]

  Fax: (028) 2222341 / 2221356

  OFISI YA MKUU WA MKOA,

  S. L. P. 299,

  BUKOBA - KAGERA.

  TANZANIA.

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  TAREHE 04 AGOSTI, 2O16

   

  Ndugu Waandishi wa Habari, Katika Mkoa wetu wa Kagera vimeibuka vitendo vya hujuma hasa wakati huu wa majira ya kiangazi (hususani mwezi Juni na Julai 2016) ambapo wananchi wenye nia mbaya na Taifa na Mkoa wetu wamekuwa wakichoma moto ovyo na kuteketeza misitu ya hifadhi ya Serikali, mashamba ya miti ya watu binafsi na mashamba ya mazao ya chakula suala ambalo halikubaliki na ni kinyume na sheria zilizowekwa  na  nchi yetu.

   

  Ndugu Waandishi wa Habari, Kwa taarifa nilizonazo za uchomaji moto katika Halmashauri za  Wilaya tatu mkoani kwetu ni kama ifuatavyo; Kufikia Agosti 3, 2016 katika  Manispaa ya Bukoba maeneo yaliyoripotiwa kuchomwa moto ni ekari tisa na nusu (9.5) zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni ishirini (20,000,000)

   

  Katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba zaidi ya ekari 473 za misitu ya hifadhi ya kupandwa na mazao ya chakula imechomwa na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha kwa wananchi.

  Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo taarifa zilizonifikia ni kwamba tayari ekari 53 za misitu na mazao ya chakula zimechomwa na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha pia kwa wananchi. Kwa hizo Halmashauri chache za Mkoa wa Kagera unaweza kuona uharibifu mkubwa wa uchomaji moto ulivyosababisha hasara kubwa.

   

  Ndugu Waandishi wa Habari, Kutokana na uharibifu huo wa uchomaji moto katika Mkoa wetu wa Kagera na kwa Mamlaka niliyopewa chini ya kifungu cha  sheria ya Tawala za Mikoa, sheria Na. 19 ya mwaka 1997 Kifungu cha 5 kifungu kidogo cha (1) na (2), Sheria hii inanipa Mamlaka na majukumu ya kulinda Amani na Usalama na kuhakikisha uzingatiaji wa sheria katika Mkoa wa Kagera unatimizwa.

   

  Aidha, kwa kuzingatia sheria ya misitu Na. 14 ya mwaka 2002 vifungu vya 70 hadi 73 na Kifungu cha 91 vifungu kidogo (1) na (2) vinavyozuia mtu yeyote kuchoma mashamba binafsi na misitu ya hifadhi. Hivyo, ninawaagiza Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya wote Mkoani Kagera kuhakikisha wanadhibiti uchomaji moto ovyo kwenye Wilaya zao kwa kutumia sheria zilizopo ikiwa ni pamoja na sheria ndogo za Halmashauri za Wilaya za utunzaji wa mazingira.

   

  Ndugu Waandishi wa Habari, Aidha, naagiza kwa maeneo ambayo yatabainika kuchomwa moto, moto huo uzimwe mara moja kwa ushirikiano wa wananchi na kumbaini mara moja mwananchi aliyehusika kuchoma moto huo katika eneo husika.

   

  Pia naagiza Viongozi wote kuanzia ngazi ya Kitongoji,Kijiji,Kata,Tarafa na Wilaya wenye jukumu la kisheria kusimamia misitu na mazingira wahakikishe waharifu wa uchomaji moto wanabainika na kukamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria, Viongozi watakaoshindwa kufanya hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

   

  Ndugu Waandishi wa Habari, Vile vile naagiza Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya kuhakikisha taarifa za kudhibiti uchomaji moto na kubaini waharifu wa uchomaji moto ovyo zitumwe Ofisini  kwangu kila siku. Pia Kamati za Mazingira zilizoundwa kupitia sheria ya mazingira ya mwaka  2004 kwa ngazi zote zihakikishe zinatekeleza kazi zake kisheria na kuwasilisha taarifa Mkoani kila Wiki.

   

  Ndugu Waandishi wa Habari, Nawakumbusheni kuwa Misitu ni rasilimali muhimu kwa Taifa na kwa Mkoa wetu wa Kagera kwani misitu ni uhai. Misitu huchangia kuwepo kwa hali nzuri ya hewa, uwepo wa mvua za uhakika na uwepo wa vyanzo vya maji vya kutosha Mkoani kwetu na Taifa kwa ujumla.

   

  Sheria ya Misitu Na. 14 ya mwaka 2002 inaitambua misitu ya hifadhi ya asili na ile ya kupandwa na inaeleza wazi ni jukumu la kila Mwananchi kuhakikisha misitu hii inalindwa na kutunzwa. Nawakumbusheni wananchi kuhakikisha wanatunza mazingira na kuacha vitendo vya uchomaji moto ovyo katika mkoa wetuHOME wa Kagera badala yake wanatakiwa kuwa walinzi mazingira katika maeneo yao.

   

   

  Imetolewa na;           Mhe. Meja Jenerali (Mst) Salum M. Kijuu

                                 Mkuu wa Mkoa

  KAGERA

  CHATO-GEITA. Msafara wa Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Dkt. Harrison Mwakyembe umepata ajali Jana July 13,2016 ambapo gari la DPP limepata ajali na kupinduka baada ya tairi la mbele kulia kupasuka,Katika eneo la Bwanga mkoani Geita wakati wa msafara ukielekea Chato kutokea Geita. Habari zainasema gari hilo limeishainuliwa na safari inaendelea. Chanzo cha ajali hiyo kinaelezewa kuwa ilikuwa kuwakwepa watoto wawili waliovuka barabara ghafla na bila tahadhali. Dereva na Abiria wote akiwemo Mkurugenzi wa makosa ya jinai Mhe. Biswalo Mganga na msaidizi wake inasemekana wametoka salama

LOCAL

MATUKIO

MICHEZO

 • AGOSTI 17, 2016 -NGAO YA JAMII

  Yanga vs Azam Taifa

  Agosti 20, 2016

  Kagera Sugar vs Mbeya City Kaitaba

  Simba vs Ndanda FC Taifa

  Toto African vs Mwadui FC Kirumba

  Stand United vs Mbao FC Kambarage

  Mtibwa Sugar vs Ruvu Shooting Manungu

  Azam FC vs African Lyon Azam Complex

  Majimaji FC vs Prisons Majimaji

  AGOSTI 21, 2016

  SERENGETI BOYS VS AFRIKA KUSINI TAIFA

  Agosti 27, 2016

  Mbao FC vs Mwadui Fc Kirumba

  JKT Ruvu vs Simba Taifa

  Kagera Sugar vs Stand United Kaitaba

  Mtibwa Sugar vs Ndanda FC Manungu

  Azam FC vs Majimaji FC Azam Complex

  Prisons vs Ruvu Shooting Sokoine

  Agosti 28, 2016

  Yanga vs African Lyon Taifa

  Toto african vs Mbeya City Kirumba

  Agosti 31, 2016

  Yanga vs JKT Ruvu Taifa

   

  KUFUZU AFCON

  SEPTEMBA 2, 2016

  NIGERIA VS TANZANIA

  Septemba 3, 2016

  Mbao fc vs Mbeya City Kirumba

  Kagera sugar vs Mwadui Fc Kaitaba

  Majimaji fc vs Mtibwa Sugar Majimaji

  Jkt ruvu vs African Lyon Mabatini

  Septemba 4, 2016

  Stand united vs Toto African Kambarage

  Septemba 7, 2016

  Simba vs Ruvu Shooting Taifa

  Prisons vs Azam FC Sokoine

  Ndanda vs Yanga Nangwanda

  Septemba 11, 2016

  Simba vs Mtibwa Sugar Taifa

  Septemba 10, 2016

  Mwadui FC vs Stand United Mwadui Complex

  Mbeya City vs Azam Fc Sokoine

  African Lyon Vs Mbao FC Karume

  Ndanda Fc vs Kagera Sugar Nangwanda

  Prisons vs Toto African Sokoine

  Yanga vs Majimaji Fc Taifa

  Ruvu shooting vs JKT Ruvu Mabatini

  Septemba 17, 2016

  Mwadui FC vs Yanga Kambarage

  Mbeya City vs Prisons Sokoine

  Mtibwa Sugar vs Kagera Sugar Manungu Complex

  Azam FC vs Simba Taifa

  Ruvu Shooting vs Mbao FC Mabatini

   Majimaji FC vs Ndanda FC Majimaji

 • IFAHAMU RATIBA YA LIGI KUU TANZANIA 2016/2017.

  AGOSTI 17, 2016 -NGAO YA JAMII

   

  Yanga vs Azam Taifa

   

  Agosti 20, 2016

   

  Kagera Sugar vs Mbeya City Kaitaba

  Simba vs Ndanda FC Taifa

  Toto African vs Mwadui FC Kirumba

  Stand United vs Mbao FC Kambarage

  Mtibwa Sugar vs Ruvu Shooting Manungu

  Azam FC vs African Lyon Azam Complex

  Majimaji FC vs Prisons Majimaji

   

  AGOSTI 21, 2016

   

  SERENGETI BOYS VS AFRIKA KUSINI TAIFA

   

  Agosti 27, 2016

   

  Mbao FC vs Mwadui Fc Kirumba

  JKT Ruvu vs Simba Taifa

  Kagera Sugar vs Stand United Kaitaba

  Mtibwa Sugar vs Ndanda FC Manungu

  Azam FC vs Majimaji FC Azam Complex

  Prisons vs Ruvu Shooting Sokoine

   

  Agosti 28, 2016

   

  Yanga vs African Lyon Taifa

  Toto african vs Mbeya City Kirumba

   

  Agosti 31, 2016

   

  Yanga vs JKT Ruvu Taifa

   

  KUFUZU AFCON

   

  SEPTEMBA 2, 2016

   

  NIGERIA VS TANZANIA

   

  Septemba 3, 2016

   

  Mbao fc vs Mbeya City Kirumba

  Kagera sugar vs Mwadui Fc Kaitaba

  Majimaji fc vs Mtibwa Sugar Majimaji

  Jkt ruvu vs African Lyon Mabatini

   

  Septemba 4, 2016

   

  Stand united vs Toto African Kambarage

   

  Septemba 7, 2016

   

  Simba vs Ruvu Shooting Taifa

  Prisons vs Azam FC Sokoine

  Ndanda vs Yanga Nangwanda

   

  Septemba 11, 2016

   

  Simba vs Mtibwa Sugar Taifa

   

  Septemba 10, 2016

   

  Mwadui FC vs Stand United Mwadui Complex

  Mbeya City vs Azam Fc Sokoine

  African Lyon Vs Mbao FC Karume

  Ndanda Fc vs Kagera Sugar Nangwanda

  Prisons vs Toto African Sokoine

  Yanga vs Majimaji Fc Taifa

  Ruvu shooting vs JKT Ruvu Mabatini

   

  Septemba 17, 2016

   

  Mwadui FC vs Yanga Kambarage

  Mbeya City vs Prisons Sokoine

  Mtibwa Sugar vs Kagera Sugar Manungu Complex

  Azam FC vs Simba Taifa

  Ruvu Shooting vs Mbao FC Mabatini

   Majimaji FC vs Ndanda FC Majimaji

 •  

 © 2016 / Radio Kwizera / All Rights Reserved / teamgraphiqs